Tuesday, February 17, 2015

REPOST: BANGO SANGHO YAWEZESHA WANAFUNZI 150 SHULE YA MSINGI KIBUGUMO KUKETI


Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akikata utepe kuzindua moja ya majengo ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO kwenye hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki Kigamboni jijini Dar. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO, Amit Nandy (wa pili kushoto) Pintu Dutta na Dipankr ambao ni wajumbe wa umoja huo. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).


WANAFUNZI 150 waliokuwa katika dhiki ya elimu shule ya msingi Kibugumo kutokana na kulazimika kusoma wakiwa wameketi sakafuni wamekabidhiwa madawati yatakayowawezesha kusoma kwa raha.

Madawati hayo yamekabidhiwa jana na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO mbele ya shuhuda ya Balozi wa India nchini, Debnath Shaw.
Pamoja na madawati hayo taasisi hiyo ilikabidhiwa madarasa mawili yaliyokarabatiwa.

Stori kutoka Michuzi blog: http://michuzi-matukio.blogspot.com/2015/02/bango-sangho-yawezesha-wanafunzi-150.html


No comments: