Wednesday, September 19, 2012

MCHANGO WAKO UNAHITAJIKA HMT KUSAIDIA SHULE YA MSINGI YA KIVULE


Mkoani Dar es Salaam, wilaya ya Ilala kuna shule ya Msingi iitwayo Kivule ambayo ina jumla ya wanafunzi 3,585; madarasa 11, waalimu 30, na madawati 300. (Kwa mujibu wa takwimu zake za Januari 2012).

Kutokana na wingi wa wanafunzi wa shule hiyo kulinganisha na rasilimali zake kama madawati, waalimu na madarasa; Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Ndalo alilazimika kuwagawa wanafunzi hao katika shifti mbili yaani wale wanakuja shuleni asubuhi mpaka mchana, na wanaokuja shuleni mchana hadi jioni. Hata hivyo, mwalimu mkuu huyo hakuishia hapo, alienda kuililia Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi ambao waliahidi kuongeza madarasa 7 hapo shuleni.

Mwalimu grace hakuishia hapo, alifika katika ofisi zetu na kuomba msaada zaidi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Alieleza kwamba, matatizo makubwa mawili yanayoishambulia shule ya msingi Kivule ni:

1.      ukosefu wa madawati ya kutosha (asilimia kubwa ya wanafunzi wakiwa wanakaa chini)

2.      Mila potofu zinazozunguka maeneo ya shule hiyo.

Hivyo mwalimu mkuu huyo ameomba misaada ifuatayo:

1.      Madawati 895 ambapo dawati moja ni shiligi 90,000/= kwa hapa Dar es Salaam

2.      Kiasi cha fedha tasilimu 200,000/= kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa waalimu ambao watajitolea muda wao kuwaelimisha wazazi wa wanafunzi hao juu ya umuhimu wa elimu; pamoja na kuwafundisha kusoma, kuandika, na kuhesabu.

 

Akifafanua juu ya tatizo la madawati alisema kuwa, kwa sasa dawati moja linakaliwa na wanafunzi 5-6 (ambapo kwaida dawati moja linakaliwa na wanafunzi 3) na bado wanafunzi wengine wanakaa chini.

Akiendelea zaidi kufafanua juu ya tatizo la pili alisema kuwa, jamii inayoizunguka shule hiyo inaamini sana katika ndoa za mapema ambapo wanafunzi hususani wa kike wakilazimishwa kuolewa au kupendelea kuolewa na kuoa baada ya kutoka jandoni ama unyagoni. Vilevile, jamii hiyo hawatambui juu ya uzazi wa mpango, kupelekea mwanamume mmoja kuwa na hadi watoto 30 na wanawake tofauti (hili linachangia uongezekaji wa wanafunzi shuleni hapo wakati rasilimali ni chache). Pamoja na hayo yote, wazazi wa wanafunzi hao hawaipi Elimu kipaumbele, hivyo msaada unahitajika kuwakomboa wazazi hao pia katika fikra potofu ili waanze kusisitizia watoto wao umuhimu wa elimu kwani ndio ufunguo wa maisha.

Hasaan Majaar Trust ingependa kushirikiana na wewe katika kuisaidia shule ya msingi Kivule. Kitakachopatikana kitapelekwa shuleni hapo na wewe kama mfadhili wa namna moja hadi nyingine utakuwa pamoja nasi kukabidhi rasilimali hizo.


Wasiliana nasi kupitia

·         simu namba:  +255 767 699932 / +255 718528009 / +255 685 353566 / +255 22 2775116

·         baruapepe:       info@hassanmaajartrust.org

 




No comments: