Thursday, May 28, 2015

Reblog: WAZIRI MKUU APOKEA VITABU KUCHANGIA SHULE ALIYOSOMA

reblog from Vijimambo blog



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea msaada wa
vitabu 895 vyenye thamani ya sh. milioni 6.5/- ikiwa ni jitihada ya wadau mbalimbali
kuchangia shule ya msingi aliyosoma ya Kakuni iliyoko kijiji cha Kibaoni,
wilayani Mlele, mkoani Katavi.

Waziri Mkuu amepokea msaada huo jana mchana (Jumanne,
Mei 26, 2015) kwenye shule mpya ya msingi Kakuni ambayo bado inaendelea
kujengwa kwenye kijiji cha Kibaoni.

Akizungumza
katika hafla hiyo fupi mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu Pinda
aliishukuru kampuni ya General Booksellers Ltd ya kutoka Dar es Salaam kwa
msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake
aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.

read more at Vijimambo blog


No comments: