Thursday, August 23, 2012

MAONI YAKO KUHUSU DUKA LA HISANI HMT (HMT Charity Shop)



SWALI:  

·         Je umeshawahi kutembelea duka lolote la hisani ndani ama nje ya nchi?

·         Nini maoni yako juu ya dhumuni la “duka la hisani?”

·         Vipi tunaweza boresha duka la hisani la HMT?

Hassan Majaar Trust ina duka la hisani lililopo ofisi zetu Dar es Salaam maeneo ya  Mikocheni Arcade bulding.  Maana halisi ya duka la hisani ni kuwa watu mbalimbali wanaleta vitu vyao kama nguo, viatu, mabegi, vyombo vya dukani na kadhalika (AMBAVYO VIPO KATIKA HALI NZURI YA USAFI NA UBORA ila ambavyo mtu huyo HAVITUMII TENA) halafu baada ya kufika hapo dukani vinauzwa kwa bei nafuu sana.

Hii inawezesha wale watu wengi wenye uwezo wa chini kujipatia vitu vyenye ubora kwa bei nafuu, na pia kwa HMT inasaidia kukusanya fedha kwa ajili ya shughuli zake mbalimbali za kuisaidia jamii.

Duka hilo linafunguliwa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi  mpaka saa kumi na moja na nusu  jioni Jumatatu hadi Ijumaa; na Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nane na nusu mchana.
Muonekano wa duka la hisani la HMT kwa nje

Ndani ya duka la hisani la HMT

Vitabu vilivyopo...

Tai nazo pia zipo

Viatu vilivyopo.
 
 
KARIBU SANA.

No comments: